1.  Juakali

Ni tamthilia bora yenye kujawa visa kadha wa kadha katika maisha kama wivu,chuki na mapenzi ya dhati na pia ni filamu iliyo onyesha matabaka mawili kati ya matajiri na upande wa watu wa kati na wale wasiojiweza lakini wakiwasilisha maudhui tofauti tofauti kulingana na uhusika maalum. Pia ni filamu pendwa ambayo inaongoza kufuatiliwa na watu wengi sana. Unaweza  kuitizama ndani ya Dstv channel namba 160 kila jumatano – jumapili saa 3 usiku.

2. Huba

Hii ni tamthilia bora nguri au kongwe kwa sasa toka mwaka 2017 hadi sasa 2022 imekuwa filamu pendwa kwa watu kutokana na visa mbalimbali haswa katika upande wa mahusiano ya kimapenzi na ndipo inazaliwa chuki na ugomvi baina ya familia mbili tofauti na kufikia hatua hadi uchawi unatumika katika kutengenzeza mambo yakae sawa na ili kupata kinacho hitajika. Inapatikana ndani ya Dstv channel namba 160 kuanzia jumatatu – ijumaa saa 3 usiku.

 

3. Moyo

Ni hii tamthilia bora iliyobeba visa mbalimbali vinavyotokana na mapenzi ambavyo ni kama Usaliti, Wivu wa kimapenzi na kuleta matatizo makubwa sana katika moyo wa binadamu na hii ikapelekea kuleta visasi baina ya wapendanao. Tamthilia hii pendwa inapatikana Chaneli ya Sinema Zetu ndani ya Azam Tv kuanzia saa 1 usiku kila jumatatu – Alhamisi

4. Pazia

Pazia ni tamthilia bora inayopendwa kwa sababu ya mtiririko mzuri wa visa vinavyotokea katika maisha haswa upande wa mapenzi. Filamu hii inaonyesha jinsi mambo mazito yanayotokea kwenye maisha lakini hayafahamiki kwa sababu yapo nyuma ya pazia lakini pazia hili linafunguka na ukweli unadhihirika. Juu ya chuki, usaliti ,Fitina na ubinafsi. Tamthilia hii inapatikana Dstv channel namba 160 kila jumatatu – jumatano saa 1:30 usiku.

 

5. Sinia

Sinia ni tamthilia bora ambayo inahusu familia mbili za hali ya juu ambazo zinaishi kwa kuficha siri za matukio yanayotendeka baina yao na kuibua mauaji,Chuki pamoja na usaliti. Pia hii filamu inaonyesha malipizi ya visasi juu ya watu au familia zenye hali ya juu yani matajiri. Na kuleta maafa kwa wasio na hatia, Ni nzuri na yenye kuelimisha katika jamii tamthilia hii pendwa inapatikana ndani ya Dstv 160 kila jumamosi na jumapili saa 3 usiku.

 

6. Maji ya shingo

Ni tamthilia  bora  ambayo inahusu kisa cha binti aliyekataa shule na kushawishika kwenda mjini kutafuta maisha mazuri. Badae Majii ya shingo yanamfika baada ya kuleta matatizo mengi na kuibuwa chuki ,wivu wa kimapenzi na vitu kadha wa kadha. Tamthilia hii pendwa inapatikana ndani ya azam tv channel namba 103 kila ijumaa na jumapili saa 1:30 usiku usikose

 

7. Yalaiti

Hii ni tamthilia bora ambayo imeanza hivi karibuni yenye kubeba maudhui mbalimbali kama Mapenzi,Usaliti na Wivu. Yalaiti ni neno lenye maana ‘Kama ningejua’ hii ni kutokana na visa vya kimapenzi vinavyotokea baina ya wapendanao haswa pale inapogundulika unaempenda nae kuna mtu anampenda. Pia inaonyesha majuto haswa baada ya kugundua unatendwa katika mahusiano. Tamthilia hii unaweza kuitizama ndani ya Dstv channel namba 160. Kuanzia jumatatu – ijumaa saa 4 usiku.

 

8. Chini ya Kapeti

Hii tamthilia yenye maudhui ya kuchekesha na yenye maisha halisi ya  uswahilini na kuonyesha vitimbwi na mambo yanayotokea uswahilini. Tamthilia hii pendwa pia ina maudhui yenye visa na mikasa ambayo inatokaea kila siku katika jamii zetu na kwenye maisha kwa ujumla ni tamthilia kali ambayo hutakiwi kuikosa.tamhilia hii inapatikana chaneli ya Sinema zetu ndani ya Azam tv.

 

9. Pini

Pini ni tamthilia bora na pendwa ambayo imebeba stori nzuri kuhusu kijana aliyefanikiwa kutoroka jeshi la polisi ili kwenda kutetea penzi lake yeye na mkewe  ambaye alitakiwa aolewe na mwanaume mwingine. Tamthilia  hii inaonyesha Upendo pamoja na Chuki katika familia na kupelekea ndugu kwa ndugu kutoaminiana na kupoteza upendo pamoja na uaminifu. Bado inapendwa na kufatiliwa na kupendwa watu wengi. Filamu hii pendwa inarushwa kupitia Channel namba 160 ndani ya Dstv.

 

10. Angel Faces

Hii ni filamu bora na pendwa ambayo imeonyesha nguvu ya  mapenzi katika maisha yetu inavyoweza kuleta Ukatili, Wivu na hata mauaji pia hii yote ni kwa sababu ya mapenzi. Tamthilia hii inayopendwa na kutizamwa na watu wengi inapatikana ndani ya StarBongo katika kisimbuzi cha Startimes saa moja usiku.

 

Pamoja kuonyesha Tamthilia hizi kumi zinazoendelea mwaka 2022 pia kuna tamthilia nyingine ambazo zinafanya vizuri kwa sehemu yake katika Channeli za televisheni kama vile Angel Faces,Kitasa pamoja na nyingine nyingi.