Ibrahim Oswald ni mwigizaji wa filamu mwenye asili ya Tanzania, ambaye anafahamika kupitia filamu ya
Hadithi za kumekucha Tunu iliyompa umaarufu kubwa baada ya kuicheza vizuri husika ya Mashoto
iliyomletea tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Tamasha la Zanzibar International Film Festival (ZIFF).
Ibrahim Osward ametoka kwenye familia yenye damu ya Sanaa, Shagazi yake alikuwa mwigizaji mahiri
katika tasnia ya uigizaji huku baba yake akiwa na talanta ya kucheza ala za muziki na kuimba.
Safari yake ya kisanii ilianza mwaka 2011 mara tu baada ya kumaliza masomo yake, akiwa na lengo la
kugundua na kukuza kipaji chake. Alianza kwa kujifunza uigizaji na kushiriki katika vikundi mbalimbali vya
Sanaa kama Jakaya Theatre ambako amefanya sana mazoezi kabla hajapewa husika kwenye michezo
mitatu tofauti na baadae kuondoka alivyoona kikundi kina legalega na kuhamia Timamu African Media,
akiwa Timamu aliamua kujikita kwenye kujifunza mambo mbali mbali nyuma ya kamera kama kufanya
uhariri na kupiga picha ikiwemo kuandaa profile za wasanii wengine wa pale Timamu.
Mwaka 2017, alipata fursa ya kushiriki katika filamu inayoitwa Tunu, iliyokuwa mradi wa kipekee
ulioongozwa na John Riber na kumshirikisha muigizaji mashuhuri Jacob Stephen. Uigizaji wake ulimletea
umaarufu na kuanza kuvutia mashabiki wengi. Filamu hii ilimsaidia kujenga jina lake katika tasnia ya
uigizaji na hata kumletea tuzo ya Mwigizaji Bora kwenye Tamasha la Zanzibar International Film Festival
(ZIFF) mwaka 2017.
Kuendelea kujaribu bila kukata tamaa ndio mbinu pekee iliyomfanya aweze kupata nafasi ya kuigiza
husika ya Mashoto kwenye filamu ya Hadithi za kumekucha Tunu. Alishiriki shindano la Tanzania Movie
Talent (TMT) mara ya kwanza Mtwara ambako alikosa nafasi, shindano likaja Dar es salaam na yeye
akarudi Dar es Salaam kushindana kwa mara nyingine pia hakupata. Mwaka wa pili akaisubiri shindano
la TMT Dar es Salaam hakupata tena. Kipindi hicho hicho cha karibu MFDI walitaka kufanya filamu
wakatumia video za mashidano ya TMT kupata Cast wa filamu ya Kumekucha Tunu. Kupitia video za TMT
za mashidano wakapata wasanii wanaowataka Pamoja Ibrahim Oswald.
Kazi nyingine alizoshiriki ni pamoja na filamu ya Bahasha yam waka 2018, tamthilia ya Single Mama
mwaka 2020 iliyorushwa kupitia chaneli ya Sinema Zetu. Mbali na filamu na tamthilia, pia alishiriki katika
uzalishaji wa matangazo ya televisheni akiwa nyuma ya kamera.
Ibrahim Oswald alitambua umuhimu wa kujifunza zaidi kuhusu utengenezaji wa filamu na alipata fursa
ya kwenda Afrika Kusini, ambapo alikutana na wataalamu mbalimbali katika tasnia hiyo na kushiriki
katika miradi ya kimataifa. Hii ilimwezesha kupanua upeo wake katika uigizaji na utengenezaji wa filamu.
Mwaka 2023 alishiriki filamu ya Lost and Found iliyotayalishwa na Henry Mwakajumba ambaye
ameandika na kuongoza filamu hiyo. Filamu hiyo tayari imezinduliwa Spain mjini Katalunya.
Kwa ujumla, Ibrahim Oswald ni mwigizaji na mtengeneza filamu anayekuwa kwa kasi katika tasnia ya
sanaa ya Tanzania, akiendelea kuleta ubunifu na ujuzi wake katika uigizaji na utengenezaji wa filamu.
List of famous pictures
2023 – Lost and found
2022 –Kosa Moja
2020 – Single Mama
2018 – Bahasha
2017 – Hadithi za Kumekucha Tunu
2016 – Mhuni
2013 – Ngoma series
“Changamoto kubwa tunayopata waigizaji chipukizi kwa bahati mbaya au nzuri ni wakati ule
tunapopata tuzo. Yaani afadhali wakati ule ambapo msanii chipukizi hujapata tuzo sababu unapopata
tu, baadhi ya wasanii waliotangulia wanapotuona katika hatua hiyo badala ya kutuunga mkono
‘wanatukunjia’, wakati huo huwa mgumu sana".
"hawajali ukweli wa kwamba sura za vipaji vipya ndio zinazohitajika kwenye soko kwa sasa, sababu
unajua kitu kikisha zoeleka kwenye macho ya watu kinakuwa cha kawaida, hivyo sura mpya zinapokuja