Huu ni mfululizo wa Watoto walioteka tasnia ya filamu Tanzania kupitia husika walizocheza katika tamthilia na filamu kwa miaka tofauti kuanzia miaka ya 1990 mwishoni mpaka sasa.
Watoto hawa ni shuhuda ya kwamba umri sio kikwazo cha kuigiza kwa kiwango cha juu katika tasnia ya maigizo,
Tunaanza na Watoto walioteka tasnia ya maigizo kuanzia mwishoni mwa miaka ya 90 mpaka miaka ya hivi karibuni.
1. Abduli
Huyu ni Abduli husika ya mtoto wa kiume ambaye alionyesha ujasiri kwa kumpinga baba yake aliyekuwa na tabia ya kumpiga mama yake na kutojali familia. Mama yake alitambulika kama Mama Abdul husika iliyochezwa vizuri na marehemu Salome Nonge.
Husika hii ilichezwa na Abdulkhadir Nzige, Hii ni moja kati ya husika za Watoto ambayo ilifanya vizuri sana kwenye Television kupitia Tamthilia inayoitwa Je Baba Utacha? Tamthilia iliandaliwa na kundi la Mambo hayo Mwaka 1997. Kipindi hicho Abduli alianza kuonekana akiwa na umri wa miaka 12.
Aliendelea kufanya filamu kama Usiku wa Giza mwaka 1998, Dhoruba mwaka 1999 na hivi karibuni Tamthilia ya Rebecca mwaka 2020.
2. Kibakuli
Kibakuli ilikuwa ni husika pendwa iliyochezwa na mtoto wa kiume kibonge anayependa kutembea na manati yake shingoni akitokea familia ya Muhogo Mchungu.Husika hii ilichezwa na sadick Mbelwa.
Tulianza kumuona Kibakuli kupitia tamthilia ya Hujafa Hujaumbika mwaka 1998 ambayo ilikuwa inaonyeshwa kupitia ITV akiwa na miaka 13. Mvuto mkubwa wa kuigiza ulikuwa pale ambapo kibakuli anaagizwa na baba yake (Muhogo mchungu) kupeleka ujumbe wa mapenzi kwa mwanamke wake wa pembeni ambaye na yeye pia kibakuli anampenda pia. Kibakuli ni moja ya husika za Watoto ambayo ilifanya vizuri katika televisheni.
Kibakuli alikuwa ni zao la kikundi cha kaole ambacho ni chanzo kwa wasanii wengi wa filamu za maigizo Tanzania.
3. Nyamayao
Nyama yao ni husika ya mtoto wa kike mwenye aiba ya aibu kutoka familia ya Muhogo mchungu. Katika thamthilia ya Fukuto, Nyama yao alichezwa ngoma katika kuandaliwa kuolewa na Mzee Pwagu.
Husika hiii ilichezwa na Happiness Stanslaus. Nyama yao moja kati ya uhusika ambao umeishi kwa muda mrefu kwa wapenzi wa filamu Tanzania. Baada ya kutoka akiwa binti mdogo aliendelea kushiriki kazi nyingine kama Usaliti, Prisoner, Kafara na Super mama (short film)
4. Anita
Salwa Mazurui maarufu kama Anitha, ni jina lililotokana na husika aliyocheza kama mtoto mbea na mnoko kupitiliza katika tamthilia ya Kizaa zaa ya mwaka 2002. Tamthlia hiyo ya Kizaa zaa iliandaliwa na kundi la Sanaa la Kidedea Arts Group.
Husika hii ya Anita ni moja kati ya husika nyingi za Watoto zilizoigiza kwa mafanikio zaidi kwenye runinga na kuishi vichwani kwa mashabiki wengi kwa muda mrefu. Uwezo mzuri wa kuigiza wa Anitha uliendelea kuonekana kwa umri tofauti mpaka utu uzima, akicheza husika mbalimbali kupitia kazi nyingine zaidi kama filamu ya Bhana Kongo mwaka 2013, The point of no return mwaka 2008, Kishikwambi mwaka 2015, Geto msoto mwaka 2016. Hivi karibuni ameshiriki Tamthilia ya Tunu 2021, Pazia na Pini 2022.
5. Elizabeth Michael
Elizabeth Michael ni muigizaji wa pekee ambaye tumemuona kwenye runinga katika kila rika alilopitia toka akiwa mtoto wa miaka 5, mwaka 2005 kupitia tamthilia ya Taswira ambayo aliigiza kama mtoto mwenye huruma anayemsaidia anko kipofu husika iliyochezwa na marehemu Steven Kanumba.
Kwa miaka mingi ameigiza katika husika tofauti katika tamthilia kama Dira, Zizimo, Baragumu na filamu kama Misukosuko, Woman of Principle, Ripple of Tears, Family Tears na Mtoto wa Nyoka.
Elizabeth Michael ni muigizaji ambaye hadi sasa anaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya Filamu, hivi karibuni tumemuona kwenye tamthilia ya Sarafu ya 2018, pamoja na Mimi ya mwaka 2021.
6. Jenifer Kanumba
Jenifer Kanumba ni moja ya husika ya mtoto yenye mafanikio Zaidi katika filamu Tanzania, husika hiyo iliyochezwa na mtoto Khanifa Daudi ambaye aliigiza akiwa na miaka 12 mwaka 2010 katika filamu ya Uncle JJ ambayo aliweza kucheza kama mtoto mbishi na mjeuri aliyekosa haki za msingi kama Elimu.
Katika kipindi hicho hicho Jenifer alifanya filamu kama This is it 2010, na After Death 2013, Pamoja na Zena na Betina.Jenifer kanumba sasa hivi tunaweza kumuona katika tamthilia ya Huba ambayo bado inaruka hewani kupitia DSTV.
7. Patrick Kanumba
Othmani Njaid alimaarufu kama Patrick kanumba pia tulianza kumuona kupitia husika yake kama Patrick katika filamu ya Uncle JJ akiigiza Pamoja na Jenifer Kanumba. Alicheza husika ya mtoto anayependwa na mjomba wake na kupewa kipaumble kwenye kila jambo haswa elimu.
Uwezo mzuri alioonyesha humu ulimrudisha tena kwenye runinga kupitia filamu ya This is it mwaka 2010 wakishirikiana kwa mara nyingine na Jenifer kanumba pamoja na marehemu Steven Kanumba. Mwaka 2011 akarudi kwenye filamu Devils Kingdom akiungana na marehemu Steven Kanumba kwa mara nyingine. Mwaka 2012 aliigiza katika mfululizo wa tamthilia za Siri ya Mtungi moja ya tamthilia yenye mafanikio Tanzania.
Hivi karibuni Patrick Kanumba ameshiriki kwenye Tamthilia Sultana, Tamthilia ya Maji ya Shingo ya mwaka 2020, Yalaiti ya mwaka 2022 ambayo inaruka kwenye runinga.
8. Jamila jaylaw (Sophia Kanumba)
Jamila jaylaw anayejulikana kama Sophia Kanumba aliyeanza kuigiza akiwa na miaka 5, Mwaka 2011 kupitia filamu ya Big Daddy akicheza husika saidizi yaani supporting actor pembeni ya Steven Kanumba. Husika yake ni moja ya husika pendwa za watoto kwenye runinga. Uigizaji wake kama mhusika mbishi na mtundu ulipendwa zaidi haswa pale alipoweza kuiba na kuendesha gari la baba yake.
Baada ya kutoka Sophia aliendelea kupata husika nyingine kama Filamu nyingine ya Without Daddy mwaka 2013 muendelezo wa Big Dady kwa heshima ya marehemu Kanumba, humu aliigiza na mama yake Steven Kanumba. Waiting Soul mwaka 2012, Maduhu 2012, Nyati Mwaka 2013, Big Mommy mwaka 2014, pamoja na Sophia’s Children ya mwaka 2015. Sasa hivi bado yupo masomoni.
9. Jalilah Jaylaw
Huyu ni dada wa Sophia Kanumba anayejulikana kwa jina la uhusika wake kwenye filamu ya Big daddy kama Jamila Kanumba. Pia ni mmoja kati ya watoto wengi ambao walianza kuigizaji akiwa na umri mdogo.
Alianza kutambulika kupitia Filamu ya Big Daddy mwaka 2011 aliyocheza kama Mtoto wa Marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa kama Baba yao. Akiwa na Mdogo wake Sophia, Jalilah alicheza vizuri katika Filamu hiyo na kupelekea kutambulika zaidi. Kwa sasa Jalilah anasoma huko nchini Australia bado yupo na atarudi kwenye Tasnia ya Filamu.
10. Mwanaafa Mwinzago
Huyu ni mtoto aliyeshinda mashindano ya TMT (Tanzania Movie Talent), Mwana afa alionyesha kipaji chake vizuri kwenye mashindano hayo na hio ikapelekea kuibuka mshinda na kupata kitita cha Milioni hamsini (50),Baada ya Mashindano hayo ya TMT
Alishiriki kwenye Filamu yake ya kwanza iliyoitwa Mpango Mbaya akishirikiana na washindi wengine wa TMT mwaka 2014.
Kama kuna Muigizaji yeyote aliyeanza kuigiza Mtoto unae mfahamu tuandikie kwenye sehemu ya comment tutamuweka wakati ujao.