Daniel Manege

Director

Personal Info

  • Birth Name: Daniel Manege
  • Residence: Dar-es-Salaam, Tanzania
Social:

Biography

Daniel Manege ni muandaaji wa filamu kutoka Tanzania aliyeshinda tuzo nyingi. Kwa zaidi ya miaka tisa, amekuwa akijihusisha na tasnia ya filamu kama mwandishi wa Script, Director na Producer akiwa na filamu zaidi ya 13 kwa sifa yake huku kazi yake ya karibuni ikiwa ni Mpiganaji. Alikua na shauku ya kusimulia hadithi za Kitanzania na Kiafrika tangu akiwa shuleni na maono yake ni kuona Historia, Utamaduni na Desturi za Mtanzania zikitambulishwa duniani kupitia filamu. Tangu 2011 lengo lake ni kujenga timu ya wabunifu yenye maono sawa na anaamini kuwa ni mbinu bora ambayo itasaidia kuboresha filamu zetu na kufikia soko la kimataifa.

Akiwa na Shahada ya Kwanza ya Uhandisi na Usimamizi wa Viwanda ndiye mwanzilishi wa Kampuni ya D-Magic Entertainment Company, Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji iliyoanzishwa mwaka 2012 yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Daniel amefanya kazi na mashirika ya kimataifa kama Media For Development International (MFDI) na Zanzibar International Film Festivals (ZIFF).

x