Happiness Peter Majige

Actress

Personal Info

  • Born: May 6, 1992
  • Place: Mwanza
  • Nickname: Happy
  • Height: 5’ 8”
  • Active: 2009 - Present

Biography

Happiness Peter Majige ni muigizaji na mtaalamu wa kudansi na kucheza miondoko yaani choreographer, aliyehitimu kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA). Msanii huyu hodari wa maigizo ya jukwaani na runinga, sanaa yake ilianza jukwaani kabla ya kutambulishwa kwenye filamu na tamthilia.

Happiness alianza kujihusisha na Sanaa ya uigizaji mnamo mwaka 2009, akijikita zaidi katika maigizo ya jukwaani akiwa mkoani Manyara kwenye kikundi cha cha Sanaa Tumaini Group kwa Zaidi ya miaka mitatu ambako walikuwa wanacheza dansi, acrobatics na theatre.

Anasema amekuwa akitembea na shauku ya kuburudisha toka akiwa mtoto akiwa shule au nyumbani. Hakujua kama atakuwa mburudishaji. Shuleni alikuwa mburudishaji mkubwa zaidi, alipokuwa akifanya kitu basi watu lazima wanaenda kumuangalia. Ingawa aliendelea kusoma shule, akiwa anaendelea kukua na yeye pia aliona ana uwezo wa kuburudisha na huko ndipo nguvu yake iliekea, anapata furaha akifanya Sanaa, anajisikia kuishi na sio kuwa mnyonge, anakuwa hai zaidi wakati wa kutuimbuiza, kuigiza au kudansi, au wakati wa kufanya kitu chochote kinachohusu Sanaa.

Haikuwa rahisi kwa Happiness kuingia kwenye taaluma ya kuburudisha, kama ilivyo kwa wasanii wengi. Kipindi ameanza maonyesho (performing arts) alionekana mhuni, malaya na amepotoka mtoto mtukutu, anasema ilikuwa ni ngumu, aligombana na familia lakini bado aliendelea. Mwaka 2009 Wazazi na familia walimuelewa alipopata safari ya kwenda Norway kuburudisha. Baada ya hapo kidogo ndio wakaanza kuona yuko serious na hii sana yake inaweza kufanya kitu. Ingawa msisitizo wa kusoma shule uliendelea kupambana moto, na ilipotokea safari za kwenda kutumbuiza anaombewa ruhusu anaenda kuburudisha akirudi anaendeleea na shule. Alivyowaonyesha ustahimilivu wa kutaka kufanya Sanaa, familia kuanza kumpa sapoti.

Mwaka 2017 alianza rasmi kujihusisha na Bongo Movie, akishirikishwa kwenye Tamthilia kama Kiu ya Kisasi ya Jacob Stephen (JB), Tandi ya Vincent Kigosi (Ray). Huku akiendelea kupata shavu kwenye tamthilia kama Mimi ya Elizabeth Michael, Ahadi ya Daniel Manege na Sinia ya Spark production. Hizi tamthiia zilichangia sana kumfanya Happiness awe na jina maarufu ndani ya tasnia ya filamu.

Anaamini hii miaka ya hivi karibuni amepata nafasi ya kuigiza kwenye tamthilia kubwa nyingi kwasababu ni wakati wake. Hii ni kwa watu wote ukiwa umejiandaa na unafanya kila kitu sahihi basi muda wako ukifika hutatumia nguvu kwenye kupata kazi nzuri za filamu.

Happiness anasema katika mchakato wa kuvaa uhusika anapenda kutulia nakuutafuta nafsi yake kwenye hiyo husika aliyopewa, anajaribu kuhusisha (relate) na mtu ambaye amewahi kumuona au mazingira ambayo yanahusiana na hiyo husika halafu hurudi na kujitafuta ndani kwake iko wapi hiyo sehemu ndani yake, je anaweza kufanya hivyo? Baada ya kutulia na kujitathimini basi anajitafuta jinsi ya kucheza hiyo husika baada ya hapo anaenda kucheza hiyo husika.

Pia hupendelea kucheza katika Sinema za vitendo (Action movies), anamtaja Fredy Kiluswa kuwa ni mtu ambaye anamchango mkubwa katika sanaa yake ya uigizaji.

Written by: Barnabas Lucas

Filmography

  • Movie Name

    Ratings

  • REDIO

    Psychological Thriller I Webisodes

    7 /10
  • Ahadi

    Drama | Tv Series

    7 /10

Trailers & Videos

trailers
x

Redio | Official Trailer

Actress

Ahadi | Official Trailer

x