Isaya Mwakalindile kutoka Mbeya mjini, anafahamika zaidi na mashabiki wake kama Jitu la msituni, ana vipawa vingi kama kucheza karate, kuruka sarakasi, kucheza mpira wa miguu na kuigiza, huku sauti yake ya kuunguruma kama mnyama wa porini kuwa moja ya kivutio kikubwa katika Sanaa yake. Alianza kupenda kuigiza toka akiwa mtoto wa darasa la pili, kipindi hicho alikuwa anavutiwa na kuangalia katuni. Mara yake ya kwanza kuigiza ilikuwa kanisani alicheza kama mungu kwenye igizo liliandaliwa hapo kanisani. Baada ya hilo Igizo aliendelea kuigiza kwenye makanisa mengi mpaka ya kijijini. Soma Zaidi
Hakuwahi kufikiri kama anaweza kuwa msanii mkubwa ila alikuwa anapenda kuigaza. Hamu ya kutamani kuigiza ilianza kujitokeza kwa mara nyingine mwaka 2009 akiwa form one, alipoenda kumtembelea nyumbani rafiki yake mkubwa Charles, ambaye alimkosa akaambiwa ameenda sehemu moja kuigiza. Kipindi hicho Isaya alikuwa hajui kama kuna makundi ya Sanaa ya maigizo, alivyoenda kumuangalia, akajiuliza ina maana jamaa anataka kuwa kama Kanumba? Kwake aliona hiyo ni ndoto isiyowezekana kwasababu tayari aliishajengewa mitazamo kuwa kusoma ndio kila kitu.
Kama mtoto wa kwanza wa kiume katika familia alikuwa anasumbuliwa na hali ya kutaka kusaidia wazazi wake, njia ambayo alikuwa anataka kuitumia ili kusaidia wazazi ilikuwa ni kupitia Sanaa ya maigizo, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imekufa ndani yake. Sababu kubwa ya kufa kwa Sanaa ndani yake ni kutokana na maneno aliyomezeshwa na wazazi kuwa kusoma ndio kila kitu. Kipindi hicho hakuna chochote alichofikiria zaidi ya kitabu na kupelekea kufa kwa matamanio ya kuigiza yaliyo ndani yake.
Kwahiyo alivyoenda kumtembelea rafiki yake alivyofika getini akaambiwa hawezi kuingia mpaka awe ni mwanakikundi, akafikiria kujiunga tu ngoja awadanganye kwani kesho asipokuja watamuona wapi? Kwahiyo akasema amekuja kujiunga ilimradi aone kinachoendelea ndani kwenye kundi. Akafanikiwa kuingia kwenye hilo kundi lililokuwa linaitwa Mapinduzi.
Alivyoingia akaona wanavyoigiza, hapo hapo ile hali ya kutamani kuigiza ambayo ilikuwa imekufa ikaamka, akavutiwa kuona jinsi walivyokuwa na umoja, wanacheka, wanafurahi, wanakoselewa, watu wanavyoumia wakikosolewa. Akaambiwa apande kuigiza, ilikuwa ni mara ya kwanza na hakufanya vibaya sababu alikuwa ana kitu anacho kwahiyo ilikuwa kawaida, akajikuta ameingia saa tisa akatoka saa kumi na mbili, yale masaa machache ni kama amerudi kwenye dunia yake ambayo mwanzo alikuwepo, kwahiyo safari ikaanzia hapo akawa anavutana na vitu viwili, Shule na Sanaa.
Upinzani kwa wazazi ulianza 2009, hakuna aliyejua kuwa kwa miaka miwili anafanya Sanaa ya maigizo kwa siri mpaka ilipokuja kuwa changamoto mwaka 2011 akiwa form 3, ilikuwaje changamoto? kambini hapo Mapinduzi ameishaiva na ameondoka kwenye kundi, huu muda ameshakuwa chizi Sanaa yaani ameishavurugwa kiasi cha kwamba ukilinganisha ndoto ya shule na ndoto kuigiza kubwa ilikuwa ndoto ya kuigiza. Kipindi hiki anaamini alikuwa hatari kwenye performance.
Performance yake ya kwanza ilikuwa kuunguruma kama kiumbe cha ajabu mbwa mwitu si mbwa mwitu, hiyo ndio staili watu wengi walimpenda nayo alikua akienda sehemu akiunguruma lazima watu watulie waulize iki ni kitu gani na kipindi hicho movie za kutisha zinafanya vizuri hapa Tanzania ni Shumireta na Nsyuka lakini yeye alikua anaamini mbona anaweza kufanya tofauti na wao, alikuwa anajiuliza kwanini jini atokee anacheka, yeye alikuwa anaamini katika staili yake ambayo yuko nayo toka udogoni.
Turudi nyuma kidogo, hii style ya kuunguruma anayo toka akiwa mdogo, akiwa shuleni alipendelea kukaa nyuma kabisa ya darasa yaani Back bencher, kipndi hicho mwalimu akiwa anafundisha yeye anaunguruma, alikuwa ana unguruma kama simba mwalimu akigeuka yeye hukausha kimya, mwalimu akiuliza nini hicho wenzake wanaomjua wanakausha, wanacheka wanamuambia afanya tena.
Kwahiyo huo uwezo wake wa kuunguruma alikuwa hajui atakuja kuutumia wapi. Alikuwa anapenda kuangalia filamu za kutisha kama Mbwa Mwitu na filamu iliyomuinspire sana ni filamu ya The Underwold, Wolfman ya mwaka 2009, hizo ni filamu alizozipenda kuangalia. Anasema alikuwa akiigiza kuunguruma kama yule mbwa mwitu anayebadilika akiunguruma.
Baada ya kundi lao la Tumaini kuvunjika wakati alikuwa na mategemeo nalo, ikamsukuma kwenda kundi jingine, siku anaingia tu anakukuta wapo kwenye mazoezi ya filamu, siku hiyo wanaume wote walikuwa wanatafuta jini mmoja anayefaa kwaajili ya filamu inayoandaliwa na kundi. Alipokaa, yeye pekee yake ndio alikuwa mgeni, kundi lilikuwa na zaidi ya watu 70. Zamu yake ikafika, hapo ni mgeni lakini akaambiwa panda kwenye Sanaa hamna mgeni. Basi akapanda mpaka kwenye stage, kwenye kuunguruma alikuwa na staili moja ya kuinama kama mbwa mwitu kile kitendo cha yeye kuinama na kukaa ile staili, watu wakaanza kucheka, mwalimu akawaambia wakae kimya wamsikilize. Basi baada ya kuinama kama mbwa mwitu akaunguruma mara ya kwanza, akaunguruma mara ya pili, akaona watu wanatingishika akajua tayari amewakamata, wameshaingia kwenye dunia yake. Akapiga sauti kubwa zaidi akainuka hadi uso ukawa unaigiza, kitu unachopenda ukifanya lazima ujikute upo dunia ya peke yako yaani kwa wakati huo yeye ndani yake alikuwa anajiona kama limnyama fulani uko nje mtu akiona anapata unacho kiona ndani.
Hapo wanapoigiza kuna kigorofa watu hukaa walivyomsikia ana unguruma wakasimama na kuogopa, waigizaji wenzake wakamwambia mwalimu cut huyo kapandisha mashetani. Majini Dar es salaam ni jambo la kawaida wakajua amepandisha mashetani, walivyokuwa wanasema yeye alikuwa anasikia, sema hawezi kusimama sababu spirit ya kwanza ukiwa mwigizaji usiache kuigiza kama mwalimu hajasema usimame. Kwahiyo mwalimu naye akaogopa akajua kweli amepandisha majini akamwambia cut na yeye aka simama.
Mwalimu akauliza, “vipi mwanangu upo freshi?” akajibu yupo fresh, mwalimu akawaambia wakae mtu anaigiza. Isarito alivyoangalia huko chini akaona watu wamesimama wakimuangalia kwa ukimya.
Mwalimu akatoa scene hapo hapo, akataka acheza kwenye story yake ambayo kila alichokiandika amekifanya mara mbili yake kwahiyo siku hiyo akachezeshwa Jini mpaka anarudi nyumbani sauti ilikuwa haitoki kabisa yaani hata ukimwambia vipi kusema poa anashindwa, sauti ilikata kabisa sababu ndo ilikua mara yake ya kwanza. Sauti kukata ilikua sababu ya mama yake kujua yeye anaigiza, mama yake alitaka kujua mbona sauti imekauka, alijaribu kumjibu mama yake lakini mama hakumsikia na hapo nyumbani kwa nje kulikuwa na uwanja wa mpira, kwahizo kelele karibu na uwanja hawakuelewana na mama kabisa. Baada ya kuona Mama kachanganyikiwa ikabidi Isarito amwandikie katika simu akamwambia mama kuwa anaigiza, mama anajua kama anaunguruma, mama alimuuliza kuunguruma ndo sauti imekata? Mama akamwambia angalia sasa sauti imekata.
Sauti yake ilikuwa haitoki kabisa yeye mwenyewe akaanza kuogopa, pale nyumbani kulikuwa na uwanja inapo fika usiku alienda uwanjani kunguruma au kuongea kwa kuunguruma alikua anaweza kuongea hivyo hivyo kwa tabu, lakini akiongea kawaida hawezi kwahiyo alichokuwa anafanya anaenda uwanjani anaunguruma baada ya siku mbili sauti ikaanza kurudi akaendelea kuifanyia mazoezi kulizoesha koo kufanya kwa ukubwa sio kama aliovyokuwa anaifanya zamani. kwahiyo akawa amezoea.
Mpaka kipindi hiki ameishapita makundi mawili baada ya kuonekana ameunguruma, mwalimu alimpenda, alikuwa ni mwalimu mwenye uzoefu aliyepita makundi mengi kwahiyo akawa mtu wake wa karibu akaanza kumfundisha vitu zaidi. Jumamosi na Jumapili alikuwa haendi shule akawa anaenda kwa mwalimu anashinda naye mpaka muda wa mazoezi akawa anajikuta amejifunza vitu vingi vingi akawa anampeleka mpaka makundi mengine huko Mbagara kipindi hicho akajikuta kwa mda mfupi ashatembea makundi zaidi ya 50 watu wote walikua wanamjua kwa staili ya kuunguruma kwaiyo akawa maarufu katika makundi na kwa watu ambao anafanya nao shooting lakini nyumbani akirudi anakula vitaa sababu Shule kidogo ilianza kuyumba.
Mwaka 2012 ukiwa ndio mwaka wake wa mwisho wa sekondari kidato cha 4, Mama na Baba yake walitengana, changamoto kubwa ikawa kutoka kwa mama ambaye anamtaka akomae zaidi kusoma shule, na wakati huo yeye Sanaa ishamuingia damuni. Mwaka huo huo akiwa kidato cha 4, darasa la mtihani wa Taifa, atakiwi kupoteza muda lakina yeye alikuwa anapotea wiki mbili bila kwenda shule.
Mama yake ni mtu wa imani sana yaani kitu akimwambia asiende asifanye, aking’ang’ania hicho kitu hakiwezi kufanyika, mama yake alishajua ameishakuwa mwigizaji, ameshamkataza sana amechoka anajua huyu hawezi kumzuia. Alikuwa akimwambia mama yake anataka kwenda kushoot, mama alimwambia usiende achana nayo, basi Isarito atanuna ila anashangaa asubuhi mama animpangia mashuka huku anamwambia asipende kwenda kwa watu bila shuka zake, anakumbuka movie ya kwanza alipewa shuka wakati anaenda kambini.
Picha linaanza mwalimu anawaambia wanaondoka usiku huo usiku wanaenda kulala kwa mganga halafu yeye amekua kwenye dini, mara wanaenda kwa mganga wanaenda kuzindika movie yake isichezewe ifanikiwe, kwahiyo picha linaendelea mganga alivyoanza kutambika akamwambia Isarito akakae nje sababu alikuwa ni imani halafu mambo mengine alikua ajaanza kwahiyo dini ilikuwepo Sanaa kwaiyo kuingia nyumba zile na wadudu wao walio kua nao inakua vitu viwili tofauti hile move ya ilifanikiwa