Madebe Athumani Mbinga (Madebe Lidai)

Actor, producer, writer

Personal Info

  • Born: March 29, 1988
  • Place: Temeke, Dar es Salaam, Tanzania
  • Nickname: Nabii Mswahili/ Madebe Lidai
  • Active: 2005 - Present

Biography

Madebe Athumani Mbinga anafahamika zaidi kwa husika yake Nabii Mswahili, hii ni kutokana na ubunifu wa kutumia vizuri lugha ya Kiswahili na misemo ambayo imekuwa gumzo kwenye filamu zake. Madebe amesheheni talanta mbali mbali ikiwemo uigizaji, uandishi wa hadithi na uandaaji wa filamu (producer), pia ni mtaalamu wa kuzungumza lugha ya alama (mabubu) huku chimbuko la sanaa kwenye upande wa familia ni kutoka kwa mama yake.

Madebe, alifanikiwa kupita kwenye baadhi ya makundi ya sanaa, ikiwa nikutaka kujenga tabia ya kuwa na uzoefu wa kuigiza. Lakini hakuishia apo tu, aijiendeleza kwa kusoma kozi fupi kuhusiana na kamera akiwa na lengo la kutamani kuwa karibu na wasanii, ili kujua soko la filamu linahitaji nini zaidi. Mwaka 2009 alimaliza kozi iyo na kuanza shughuli za kupiga picha ndipo hamasa ya kuwa mzalishaji filamu (producer) ilipoanza, na mwaka huo huo akafanikiwa kutengeneza filamu mbili akiwa kama producer ambazo ni “From Grave” haikufanikiwa kutoka, na “Jeneza” ikiwa ni filamu yake ya kwanza iliyomtambulisha Madebe kwa mashabiki zake huku kampuni ya Balance Game ikisimamia kazi iyo.

Mwaka 2014 akarudi tena kwenye kiwanda cha filamu baada ya kimya cha mda mrefu kutokana na changamoto za kifamilia, ndipo mwaka huo akafafanikiwa kutengeneza filamu tatu ambazo ni “Kigoli”, “Mwiko” na “Mzee Ngadu” akigusa zaidi tamaduni za upwa wa Pwani na filamu zote zikaingia sokoni na kuendelea kufanya vizuri.

Madebe alitamani kufanya kitu kikubwa zaidi, ndipo mwaka 2015 alitengeneza filamu mbili ambazo ni ”Hulka” ikigharimu kiasi kikubwa ukilinganisha filamu ambazo alitoa kabla, na filamu ya “Kasumba” iliyofanya vizuri sana na kupelekea kupata tuzo ya mwandishi bora huko nchini Kenya na kujizolea mashabiki wengi nje ya nchi. Lakini pia mwaka 2016 alitengeneza filamu ya “Msungo” ambayo iligusa maisha halisi ya baba yake mzazi, hivyo ikawa ni miongoni mwa filamu aliyoiandika na kucheza kwa hisia kubwa sana, ndipo jicho la wakenya likamulika hadi Tanzania na kupitia filamu hiyo akachukua tuzo ya uandishi bora.

Hakuishia apo tu aliandaa tamthilia ya “Nabii mswahili” na kufanikiwa kutoa sehemu ya 1 hadi ya 4 mwaka 2016, na baada ya kufika mwaka 2017 soko la filamu Tanzania alimaarufu kama Bongo Movies lilionekana kushuka na muitikio wa kuuza filamu ulikuwa ni mdogo. Ndipo Madebe akafanikiwa kutengeneza filamu ya “Inshallah” na kuuza kwa kiwango cha chini kabisa tofauti na ilivyodhaniwa kuuzwa kwa filamu moja, nakujizolea hadhira wengi kutokana na bei rafiki.

Mwaka 2018 akatoa mwendelezo wa tamthilia ya “Nabii Mswahili” ikiwa na sehemu ya 5 mpaka ya 8, hivyo hivyo sehemu ya 9 mpaka 10 alizitoa mwaka 2019 na baadaye akamalizia sehemu ya 11 mpaka ya 13 mwaka 2020. Lakini pia alishiriki kwenye filamu kama Mama Mwali iliyochukua tuzo za Sinema zetu kama Best actor za mwaka 2020, Kiberiti, Kasumba, Kisiki, Wali wangu na nyenginezo nyingi.

Nguli huyu wa filamu Tanzania akiendelea kuamini kwenye kuzalisha vipaji ambavyo vitaamini kwenye utamaduni na kutengeneza filamu zenye kulenga utamaduni nchini.

Watoto (4)

    Shadrack
    Yusra
    Fahima
    Bossi

Trade Mark

    Mzee wa Misemo

Quotes

    “Waambie wali wale waje wale wali wao”

    “Chania Chanuo chenye chanio”

    “Tuongee huku Tukitunza kumbukumbu.”
    Wali Wangu – Madebe Lidai

Filmography

Trailers & Videos

trailers
x

Kiberiti | Official Trailer

Actor, producer, writer

Chanuo | Official Trailer

Barua Kwa Mungu | Official Trailer

Jasiri | Official Trailer

Insha - Allah | Official Trailer

Mama Mwali | Official Trailer

Joka La Kijiji | Official Trailer

x