Stella Mbuge ni muigizaji mlimbwende kutoka Tanzania na mshindi wa Miss Dar Indian Ocean 2011 na Miss Kinondoni 2011, muigizaji wa filamu na tamthilia kutoka Tanzania aliyecheza husika kadhaa zenye mvuto kuanzia mwaka 2020 na kupelekea kupata husika zaidi kwenye runinga. Tumeona husika zake kwenye tamthilia kama Shilingi, Danga, Moyo na Kosa moja.
Mapenzi ya kuigiza yalianza kutokana na msukumo wa ndani kabisa wenye shauku ya sanaa, ingawa pia watu wengi kwa nyakati tofauti walimshauri aingie kwenye taaluma ya kuigiza. Stella ni mmoja wa wasanii wachache wenye bahati ya kukutana na watu sahihi kwa muda sahihi, mwaka 2011 kupitia mashindano ya miss kinondoni ndipo alipoanza kukutana na watu sahihi watakaopelekea ndoto yake kutimia.
Mahusiano na Bongo Movie yalianza kipindi akiwa kwenye fainali ya tamashala la miss kinondoni ambako Yusuph Mlela na Jackline Wolper walikuwa ni wageni waalikwa kwenye tamasha hilo la kumtafuta Miss Kinondoni na kumuongezea ushawishi wa kuingia kwenye tasnia ya uigizaji. Baada ya kushiriki kwenye masuala ya ulimbwende, moja kwa moja aliingia kwenye tasnia ya uigizaji, nakufanya kazi kubwa kipindi hicho kama Nakwenda kwa Mwanangu mwaka 2012 filamu iliyoongozwa na Jacob Stephen (JB). Poor minds iliyoongozwa na Leah Mwendamseka mwaka 2013.
Mwanzo haukuwa rahisi kwa Stella katika kipindi hicho cha mpito kwa tasnia ya filamu ambayo taratibu ilikuwa inatoka kwenye mfumo wa zamani wa usambazaji wa maudhui ya filamu na kuanza kuingia kwenye mifumo ya kidigitali. Kipindi hiki kilikuwa ni kigumu kwa wasanii wengi ikiwemo Stella ambaye alisimama kuigiza na kurudi tena mwaka 2020 kupitia tamthilia ya Danga.
Mwaka 2020 akafanikiwa kushiriki kwenye tamthilia ya Shilingi iliyotayarishwa na Omary Hassan na kurushwa Azam televisheni, huku akisema ni miongoni mwa husika ngumu alizowahi kupewa. Mwaka 2021 alishiriki tena kwenye tamthilia ya “Danga” iliyoongozwa na Idris Sultan na kurushwa kupitia kisimbuzi cha Dstv, na ndipo tamthilia hii ikampa shavu kushiriki kwenye tamthilia nyingine ya Moyo mwaka 2022, hii ni kutokana na kipaji alichokionesha kwenye husika alizopewa.
Mwaka 2022 alicheza husika ya muigizaji mkuu katika tamthilia ya Kosa Moja iliyoongozwa na Christina Pande na kurushwa kupitia Azam kwenye chaneli ya Sinema zetu.
Catrina Ghati.
Nathaniel Wadak.
Sanaa ni kazi, sanaa ni pesa
Movie Name
Ratings
Drama