CineBox
Admin CineboxOctober 3, 2023Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar linatangaza Mwongozaji Mfilamu maarufu Amil Shivji kama Mkurugenzi Mpya wa Tamasha. Muongozaji maarufu wa filamu, Amil Shivji, anachukua uongozi kutoka kwa mkurugenzi wa ZIFF anayeondoka. Profesa Mhando alisema ameamua kuachia ngazi ili kuwapa fursa kizazi kijacho chenye maono.
“Sinaondoka kwa sababu ya uchovu, bali ni kuwapa vijana fursa,”
Kwa upande wake, mkurugenzi mpya wa ZIFF aliyeteuliwa alisema yuko tayari kuleta mabadiliko na kuhakikisha vipaji na uwezo wa Tanzania unajulikana kimataifa.
Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), maarufu kama Tamasha la Nchi za Dhow, ni tamasha la kila mwaka linalofanyika Zanzibar, Tanzania, na moja ya matukio makubwa ya kitamaduni katika Afrika Mashariki. [...]
Read more...
Admin CineboxSeptember 15, 2023Review ni hakiki ambazo watumiaji wetu huwasilisha kwenye tovuti yetu moja kwa moja na huhifadhiwa ndani ya database. Zifuatazo ni hatua rahisi za kufanya Review.
Login
Hakikisha umeanza kwa kubonyeza button ya “Login” juu kwenye kichwa cha ukurusa. Kisha ingia kwa kutumia akaunti yako itayokuruhusu kuacha review.
Join Today
Kama bado hujatengeneza akaunti ndani ya tovuti ya CineBox, bonyeza “Join Today” kuweza tengeneza akaunti kwa kujaza form utayopewa. Kisha bofya, “Register”.
Review
Kisha tafuta Filamu, shuka chini baada ya maelezo ya filamu na uchague nyota kati ya 1 hadi 10 kuashiria ubora wa filamu. Pia unaweza acha maoni ya kina kwenye comment, kisha bofya “Send”.
Wasilisha Filamu Unaweza kuwasilisha filamu kutumia njia zifuatazo zipate kuwa sehemu ya CineBox. [...]
Read more...
Cinebox DatabaseAugust 31, 2023Isaya Ryoba anaungana na CineBox kuzungumzia ushindi wake wa muigizaji bora mwaka 2023 wa Zanzibar International Film Festivals kutokana na husika aliyoigiza katika Filamu ya Nakupenda. Anajadili jinsi alivyochukua changamoto ya kucheza mtu mlemavu na kufanya kazi na waigizaji wengine wa filamu hiyo. Zaidi ya hayo anazungumzia jinsi ambayo amewekwa wakfu baada ya kukabidhiwa tuzo. [...]
Read more...
CineboxAugust 18, 2023Tamthilia ya Juakali imepata Muigizaji mpya ambaye ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pindi Chana. Muongozaji wa Tamthilia hiyo @lamataleah ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram,
“Asante Sana Waziri Wa Utamaduni,Sanaa Na Michezo Mheshimiwa balozi Pindi Chana kwa kuwa guest cast wa tamthilia yetu pendwa ya juakali, tunafurahia uwepo na mchango wako Katika kuburudisha na kuelimisha jamii kupitia ndani ya Maisha Magic Bongo”. [...]
Read more...
CineboxAugust 14, 2023BODI YA FILAMU YAFUNGUA DIRISHA LA KUPOKEA FILAMU KWA AJILI YA TAMASHA LA TUZO ZA FILAMU 2023
Akizungumza katika ufunguzi huo uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2023 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amesema lengo la uwepo wa Tamasha la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa Wasanii na Wadau wote wa Filamu katika eneo hili la Filamu, kutambua vipaji vyao, kuwaongezea hamasa ya kuzalisha kazi nyingi zaidi za Filamu, kuwaongezea hamasa ya kuandaa kazi zenye ubora zaidi ili wawe na ushindani mkubwa ndani na nje ya Nchi, na kusisimua fursa za uwekezaji katika eneo hilo la Filamu nchini.
Zoezi la upokeaji Filamu zitakazo shiriki katika Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2023 limeanza rasmi tarehe 11 Agosti 2023 na litadumu kwa wiki 6 hadi tarehe 25 Septemba 2023 ambapo Filamu zitapokelewa kwa njia Tatu ikiwemo, kuwasilishwa Ofisi za Bodi, Kwa njia ya Mtandao – https://taffa.info (mfumo utafunguka tar 17 Aug), pamoja na kuzifuata (Filamu) Mikoani katika mikoa 26 Tanzania Bara.
Filamu zitakazo pokelewa zitahakikiwa na Majaji na zitakazopita katika Mchujo wa kwanza zitapata nafasi ya kuoneshwa kwa hadhira ili kupigiwa kura kupitia kituo cha Azam TV Chaneli ya Sinema Zetu (103), pamoja na vituo vingine vitakavyopenda kuonesha kazi hizo. Kura zitapigwa kwa njia mbili: njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS), na kupitia mfumo wa kidijiti (https://taffa.info). Aidha, maelekezo mengine ya namna ya kupiga kura yataendelea kutolewa baada ya Mchujo wa kwanza kupitia mitandano ya kijamii ya Bodi ya Filamu.
Pamoja na mambo mengine, Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2023 limeongeza wigo wa ushiriki wa Filamu kutoka Nchi za Afrika Mashariki ambazo zimeandaliwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuendelea kuithamini na kuikuza lugha hiyo ambayo ni moja ya nembo ya Taifa letu. [...]
Read more...
Admin CineboxAugust 12, 2023Kamati ya kuchagua Filamu ya Oscars Tanzania inatoa wito kwa watayarishaji wa filamu kuwasilisha filamu zao kwaajili ya Tuzo za 96 za Oscars.
Vigezo vya kushiriki kwenye tuzo za Oscars.
Ili filamu iweze kushiriki katika Tuzo za Oscars kwenye kipengele cha Filamu Bora ya Kimataifa (International Features Film), inatakiwa iwe na vigezo vifuatavyo.
Filamu iwe imetayarishwa nje ya Marekani;
Filamu iliyooneshwa kwenye nchi husika kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Disemba, 2022 had 31 Oktoba, 2023 na ionyeshwe kwa angalau siku saba mfululizo katika kumbi za sinema za kibiashara kwa faida ya mtayarishaji na muoneshaji.
Filamu iwe imetangazwa (Promotion)/ imeonyeshwa katika kumbi za Sinema;
Filamu iwe na urefu kuanzia dakika 40;
Filamu iwe imetumia lugha nyingine mbali na kiingereza kwa Zaidi ya 50%, ikiwa na Subtitles za kiingereza;
Filamu iwe katika muundo wa Digital Cinema Package (DCP) kwa ubora wa angalau 2040 kwa 1080 pixels (2K);
Filamu iwe na sauti ya kipimo cha 5.1 au 7.1, au iwe nyenye chaneli 3 za Sauti (left, right & centre).
Angalizo: Filamu ambazo zilisambazwa au kufanyiwa maonyesho nje ya kumbi za Sinema hazikidhi vigezo kwenye Tuzo hizi. Maonesho hayo kwa umma ni:
Filamu kuonyeshwa kwenye Cable Telesheni;
Filamu isiwe katika PPV (Pay-Per-View) Video in Demand;
Filamu isiwe kwenye usambazaji wa DVD; na
Filamu isiwe imeonyeshwa/ imesambazwa kwenye ndege.
Kusambaza kwenye mtandao wa Internet.
Waandaaji waFilamu nchini wanaalikwa kuwasilisha filamu zinazokidhi vigezo vya ushiriki wa Tuzo hizi za Oscars ili ipatikane filamu moja itakayowasilishwa kwa waendeshaji wa Tuzo hizo nchini Marekani.
Tarehe za kupokea Filamu
Kamati itaanza kupokea filamu kuanzia tarehe 10 Agosti, 2023 hadi Tarehe 15 Septemba, 2023. Link za filamu zitawasilishwa kupitia: tanzaniaoscars@gmail.com. Kwa taarifa Zaidi, tembelea: Tanzania_oscars @instagram, @twitter, @facebook
NB: Kwa Maoni au Maswali Tafadhali tuma Baruapepe kwenda: tanzaniaoscars@gmail.com
imetolewa na
Dkt Mona Mwakalinga
Mwenyekit wa Kamati
10/08/2023 [...]
Read more...
Cinebox DatabaseJuly 28, 2023Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hyat Regence Jijini Dar es Salaam, ukihusisha waandishi wa habari na wadau wa filamu Tanzania katika uzinduzi wa tamthilia mbili mpya, ”Mtaa wa Kazamoyo” yakwake Dr Cheni na ”Lolita” ya william Mtitu, zitakazoanza kuonekana Agosti 04 na Agosti 14 mwaka huu zikichukua nafasi za tamthilia, “ Fungu langu” na ”Jeraha” zinazorushwa kupitia kisimbuzi cha Azam ndani ya chaneli pendwa ya Sinema zetu.
Huku tamthilia hizo mpya zikisheheni watu wengi maarufu wa tasnia hiyo ya uigizaji wakiwemo Denis Komba ,Chris Mziwanda, Genevieve Nnaji, Careen Simba na Angle Dickson kwenye “Lolita”, na vile vile kwa upande wa “Mtaa wa Kazamoyo” imehusisha watu kama Dr Cheni, Nyama Yao na Amina Ahmed.
Moja ya mtayarishaji wa kazi hizo, Dr cheni, alisema kwamba haikuwa rahisi kupeleka kazi Azam Tv kwa kuwa iliwabidi wafanyie marekebisho kidogo ya kazi yao, ili kukidhi maadili na utamaduni wa kitanzania. Pia aliwahasa wakongwe katika filamu kuwapa nafasi vijana ili waweze kuonesha vipaji vyao.
Kwa upande wa Azam Tv, mkuu wa chaneli ya simema zetu Sophia Mgaza aliendelea kutoa rai kwa waandaaji waweze kuhakikisha wanasimamia ubora wakazi zao, huku Azam Tv ikijipanga kuanza kupokea filamu kutoka kwa watayarishaji na waandaaji wa kazi hizo kupitia mfumo rafiki utakao tangazwa hivi karibuni. [...]
Read more...
CineboxJuly 24, 2023Dili za Mchongo ni filamu inayohusu uhasama kati ya magenge matatu ya mtaani yaani Genge la Mazombi ambalo linaongozwa na Biggie husika inayochezwa na Norriega Francis, Genge la wasogeza unga wasio na huruma la Chatara likiongozwa na wanzuki husika inayochezwa na Dark Master, Pamoja na genge la Nyati ambalo nalo linasogeza unga. Play boi Sizwe, muuza nyama anayependa mapenzi anajikuta katikati ya twimbili hili la magenge yasiyo na huruma. Filamu ya Dili za Mchongo imetayarishwa na Bongohoodz Pichaz ikiwa imeongozwa na Novatus Mugurusi ilitoka December 2022, kama trademark yao wammeendelea kutumia wasanii wakongwe wa bongo flava ambao wameigiza kwa ustadi mkubwa.
Dili za mchongo inakuonyesha jinsi magenge ya mtaani yanavyofanya kazi na Maisha yao ya kila siku yapo vipi. Dili ya Mchongo ni moja ya filamu za bongo movie ambayo imepiga hatua kubwa kabisa katika kujaribu kukuonyesha life style ya wahuni wanaoishi kwenye magenge nakuona jinsi ambavyo hawana huruma katika makoso ikiwemo usnichi. Kwenye Dili za mchongo utafurahia sana kuona mapenzi ya wahuni yanavyoendeshwa, inaitaji ustaadi mkubwa kuweza kujenga mapenzi katika ya genge la wahuni, kama unavyoambiwa wahuni sio watu wazuri.
Nguvu ya genge kuweza kufanya kazi ni hofu, basi ukizma kwenye filamu hii ya Dili ya Mchongo utaona jinsi ambavyo hofu inatumika vizuri katika kufanya mambo yatokee. Genge bila hofu hakuna Genge. Inaweza kuwa hofu ya umauti au hofu ya kukaa kitaa kukufakisha bila msaada wa mtu yeyote. Kwahiyo Hofu imetumiwa vizuri kwenye hii filamu. Mapenzi yana run dunia, Mapenzi yana run dunia ooooh!! Mapenzi ndio yanafanya dunia itembee, ila ukiwa kwenye magenge au mhuni basi unahitaji ustaadi mkubwa katika kujenga penzi. Kwenye pesa usnitch upo, kwenye pesa nyingi zaidi usnitch ni mkali zaidi, kwenye biashara ya dawa ya kulevya usnitch ni mkubwa zaidi, filamu nzima ya Dili ya Mchongo ni kuhusu snitch mmoja aliyendani ya genge la wasogeza unga,
Ukizama katika Dili za Mchongo itakupeleka katika dunia ambayo huijui na utajionea jinsi gani kitaa kinaweza fakisha mtu yeyote, sio poa mzee. Usikose kutazama hii another one kutoka kwa Rrhac.
[...]
Read more...