Tamthilia ya Juakali imepata Muigizaji mpya ambaye ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pindi Chana. Muongozaji wa Tamthilia hiyo @lamataleah ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram,

“Asante Sana Waziri Wa Utamaduni,Sanaa Na Michezo Mheshimiwa balozi Pindi Chana kwa kuwa guest cast wa tamthilia yetu pendwa ya juakali, tunafurahia uwepo na mchango wako Katika kuburudisha na kuelimisha jamii kupitia ndani ya Maisha Magic Bongo”.