Maunda Zorro kama baba na kaka yake alikuwa ni moja kati ya wasanii wachache ambao waliweza kumudu kufanya filamu na muziki. Vibao Maunda Ally Zorro alikuwa msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye ametokea kwenye familia iliyobarikiwa vipaji lukuki. Alikuwa mtoto wa mkongwe wa muziki wa dance, Zahir Ally Zorro na mdogo wa nyota wa bongo fleva Banana Zorro ambao wote pia ni waigizaji wa filamu.
Nyimbo zake maarufu ni Pamoja na Mapenzi ni ya Wawili na Hello ambayo ameshirikishwa na Hussein Machozi.
Enzi za uhai wake Maunda Zorro alicheza filamu kama Confusion in Rock City mwaka 2009 ambayo inahusu ndugu wawili ambao wametengana kwa Zaidi ya miaka 25. Alishiriki filamu nyingine ya Happy Couples ambayo Maunda alicheza kama mwanamuziki aliyekuwa anashinikizwa kuolewa na rafiki wa karibu wa kaka yake, bila kujali yeye anampenda nani?
Filamu nyingine ni Comedy drama Room no 13 ambayo alishiriki Pamoja na Marehemu Amri Athumani maarufu kama King Majuto, Bond Bin Sinnan Pamoja na Mzee Hashim Kambi.
Tasnia ya filamu Tanzania itaendelea kuutambua mchango wake katika Sanaa ya maigizo. Endelea kutufuata Youtube