Dili za Mchongo ni filamu inayohusu uhasama kati ya magenge matatu ya mtaani yaani Genge la Mazombi ambalo linaongozwa na Biggie husika inayochezwa na Norriega Francis, Genge la wasogeza unga wasio na huruma la Chatara likiongozwa na wanzuki husika inayochezwa na Dark Master, Pamoja na genge la Nyati ambalo nalo linasogeza unga. Play boi Sizwe, muuza nyama anayependa mapenzi anajikuta katikati ya twimbili hili la magenge yasiyo na huruma. Filamu ya Dili za Mchongo imetayarishwa na Bongohoodz Pichaz ikiwa imeongozwa na Novatus Mugurusi ilitoka December 2022, kama trademark yao wammeendelea kutumia wasanii wakongwe wa bongo flava ambao wameigiza kwa ustadi mkubwa.
Dili za mchongo inakuonyesha jinsi magenge ya mtaani yanavyofanya kazi na Maisha yao ya kila siku yapo vipi. Dili ya Mchongo ni moja ya filamu za bongo movie ambayo imepiga hatua kubwa kabisa katika kujaribu kukuonyesha life style ya wahuni wanaoishi kwenye magenge nakuona jinsi ambavyo hawana huruma katika makoso ikiwemo usnichi. Kwenye Dili za mchongo utafurahia sana kuona mapenzi ya wahuni yanavyoendeshwa, inaitaji ustaadi mkubwa kuweza kujenga mapenzi katika ya genge la wahuni, kama unavyoambiwa wahuni sio watu wazuri.
Nguvu ya genge kuweza kufanya kazi ni hofu, basi ukizma kwenye filamu hii ya Dili ya Mchongo utaona jinsi ambavyo hofu inatumika vizuri katika kufanya mambo yatokee. Genge bila hofu hakuna Genge. Inaweza kuwa hofu ya umauti au hofu ya kukaa kitaa kukufakisha bila msaada wa mtu yeyote. Kwahiyo Hofu imetumiwa vizuri kwenye hii filamu. Mapenzi yana run dunia, Mapenzi yana run dunia ooooh!! Mapenzi ndio yanafanya dunia itembee, ila ukiwa kwenye magenge au mhuni basi unahitaji ustaadi mkubwa katika kujenga penzi. Kwenye pesa usnitch upo, kwenye pesa nyingi zaidi usnitch ni mkali zaidi, kwenye biashara ya dawa ya kulevya usnitch ni mkubwa zaidi, filamu nzima ya Dili ya Mchongo ni kuhusu snitch mmoja aliyendani ya genge la wasogeza unga,
Ukizama katika Dili za Mchongo itakupeleka katika dunia ambayo huijui na utajionea jinsi gani kitaa kinaweza fakisha mtu yeyote, sio poa mzee. Usikose kutazama hii another one kutoka kwa Rrhac.