Karibu CineBox na hii ni Movie Review, na leo tunaifanyia Review Filamu ya Obambo.

Obambo ni Filamu ya kutisha au horror inayohusu Mzimu unaolipiza kisasi kwa kuua watu waliopanga kwenye nyumba ya Suleimani Machora, Unadhani nini chanzo cha mzimu huu kufanya yote haya na kwanini unaua watu wote wanaohamia kwenye nyumba hio? Kaa kwa kutulia kwani Majibu ya maswali yote haya utayapata ndani ya Filamu ya Obambo,

Obambo ni moja ya filamu bora Zaidi ya kutisha iliyozalishwa hapa Tanzania, kama mtazamaji kuna mengi ya kuburudisha ikiwemo kupata hofu ya hali ya juu na mkazo au stress katika mazingira ya kutisha kama ambavyo filamu za genre ya horror zinavyofanya.

Ustadi huu wa kuileta filamu ya Obambo katika Maisha ndio uliofanya filamu hii kuchaguliwa katika kipengele cha filamu bora ya Kiswahili katika tuzo za African Magic Viewer’s choice Awards mwaka 2022 uongozaji mzuri umefanywa katika hii filamu na kukuacha wewe mtazamaji kuweza kuhusiana na matokeo ambayo mtazamaji anaangalia.

Mvuto mkubwa katika filamu hii ya kutisha utaendelea kuupata kutokana na upigaji mzuri wa picha ambazo zimeleta uhalisiana na mvuto wa halisi wa mazingira ya kiafrika.

Sifa kubwa ya filamu za kutisha ni kuonyesha Angala la kutisha, hali Fulani ya mazingira ya kutisha kwa njia ya muziki, muundo wa sauti, mwanga na mtindo wa uhusishaji. Kwenye filamu ya Obambo sauti imeweza kutumika vizuri katika kujenga lile anga la kutisha.

Husika ya mzimu wa Obambo ambayo ilichezwa na Isaya Mwakalindile ni moja ya kishawishi kikubwa kwanini hii ni filamu ambayo unatakiwa kuiangalia mwaka huu.

Wahusika wasaidizi kama Issa Maproblem, Tony Mkongo, Mkaliwenu Original, domosi jogoo na Dankan. Hili ni zao zuri la waigizaji wazuri wanaoweka alama zao kwenye tasnia ya filamu kutokana na uwezo wao mzuri wa kuigiza genre tofuati na kuwaona wote kwa Pamoja kwenye filamu hii ya Obambo na kuweza kujichanganya vizuri ni jambo la kuvutia sana kuona.

Tumefika tamati ya review hii asante kwa kunipa time yako, pia usisahau kusubscribe chaneli yetu ili uwe wa kwanza kupata taaria zetu zote, asanteni.