Filamu hii inamuhusu mama mmoja aliyekuwa na watoto wawili Tausi na kaka yake Mazanda. Kutokana na haliduni ya kimaisha mama Mazanda aliamua kwenda kwa mganga ili kujipatia kipato kwa njia ya sangoma, ndipo mganga alimpatia hitaji lake kwa mashariti ya kutojenga nyumba nzuri yaani ya kisasa na kutoamisha biashara kutoka eneo moja kwenda lingine, kama unavyo fahamu biashara au nyumba unayo ishi inahitaji marekebisho kila baada ya wakati fulan. Hiyo hali ilimkuta mama Mazanda baada ya biashara kuwa kubwa akajikuta akitanua biashara kwa kupanga maeneo mengine ili kuwafikia wateja wake kwa wepesi zaidi. Ndipo majini yakageuka na kumpa adhabu mumewe, akawa nyoka mkubwa asie na mfano ili kumkumbusha masharti. Mtafaruku mkubwa ulitokea pale kijijini, nyoka akawa anakula watu na kuwa tishio. Kila mtu aliejua kuwa kuna nyoka hapo kijijini alimezwa na kupotea kabisa na nyoka huyo alikuwa akiishi kwenye nyumba ndogo chumbani kwa mama Mazanda, sababu iliyomfanya Tausi na kaka yake Mazanda kukimbilia kwa mjomba yao kijiji kingine. Ndipo mama Mazanda alirudi kwa mganga ili kuepusha balaa hilo lakini haikusaidia, mpaka pale kaka yake ambae nae alikuwa mganga alipokuja kumaliza tatizo hilo la nyoka-mtu anaemeza watu alipo hamia kijijini kwake.
Assistant Director: Keyto Kae
Camera: Rama Biola
Visual Effects: Kudra Abdulaziz ‘Vortex’| Sultan Tamba | Kuyonza kini
Sound Recording: Rama Bialo
Location Manager: Nassor Thomas
Production Manager: Nassor Thomas
Reviews ( 0 )