Nyota wa Bongo Movie Mlafi |Hassani Kazoa

Karibu CineBox, Kuna mambo mengi huwa yanafanyika ikiwa kama sehemu au utamaduni wa Waswahili, kama Uchawi, Kupiga Chabo, Kupiga umbea na mambo mengine mengi lakini Moja kati ya sifa kubwa ya watu wanaoishi uswahilini ukiachana na zote ni kula, kila mtaa utakuta una watu wao ambao kwenye swala la Msosi au kula wako vizuri sana na wanakula sana.

Sasa leo ninakuletea moja kati ya waigizaji maarufu ambao husika zao zimewapa umaarufu sana kwenye upande wa kula sana au kufukia misosi na hapa namzungumzia mjomba Kazoa, Huyu ni muigizaji ambae amepata umaarufu kutokana na husika yake ya kula sana au maarufu unaweza ukamuita Tonge Mbili ama Mr.Food , yani akipiga mikono yake miwili tu anazikata chipsi za buku mbili chapu, Ungana nami kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Sasa kabla ya sisi kumfahamu kama Mr Food, huyu mwamba aliwahi kuigiza Filamu kadha wa kadha pamoja na tamthilia, ikiwemo Samaki Mchangani 2013, Tamthilia ya Siri Ya Mtungi  ya mwaka 2012, Mzururaji ya mwaka 2015 , Bahasha mwaka 2018, Jambo na Vijambo Season 1 ya mwaka 2013, Jambo na Vijambo Season 2 ya mwaka 2018,  pamoja na Filamu ya Kazoa ndani ya Imani 2018.

Lakini kwa leo tutaangazia husika yake kubwa na maarufu sana hapa nchini, hapa ninazungumzia husika ya Kulakula au Mr.Food au mzee wa mapochopocho, Hassani kazoa Tulianza kumuona katika mfululizo wa kipindi cha jambo na vijambo akija na husika tofauti kabisa ya Cha Uroho,  Ndani ya kipindi hicho Kazoa alijizolea umaarufu na kupendwa na watu kwa sababu ya tabia yake ya kula sana yani anakula na kula tena …… Alafu ukimuuliza mwamba anakwambia yeye huwa hashibi,

Ila pia husika hio anayotumia imetokea kupendwa na watu kutokana na jinsi anavyo ongea ….. naweza kusema lafudhi yake anayotumia katika husika yake imetokea kupendwa sana na huwezi kuifananisha na mtu mwingine mfano.

Kwenye hii Filamu ya Kazoa Ndani ya Imani utacheka sana kwani kuna vitu vingi vilivyojawa na burudani  ambavyo amevifanya huko kama bado hujaitizama Filamu hii basi unaweza kuipata kwenye YouTube Channeli yake ya Mr Kazoa.

Unaweza kutuambia kwenye sehemu ya comment, Hassan Kazoa au Mr. Food unamkubali kwenye Filamu ipi kati ya unazo zifahamu?.