Kamati ya kuchagua Filamu ya Oscars Tanzania inatoa wito kwa watayarishaji wa filamu kuwasilisha filamu zao kwaajili ya Tuzo za 96 za Oscars.

Vigezo vya kushiriki kwenye tuzo za Oscars.

Ili filamu iweze kushiriki katika Tuzo za Oscars kwenye kipengele cha Filamu Bora ya Kimataifa (International Features Film), inatakiwa iwe na vigezo vifuatavyo.

  • Filamu iwe imetayarishwa nje ya Marekani;
  • Filamu iliyooneshwa kwenye nchi husika kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Disemba, 2022 had 31 Oktoba, 2023 na ionyeshwe kwa angalau siku saba mfululizo katika kumbi za sinema za kibiashara kwa faida ya mtayarishaji na muoneshaji.
  • Filamu iwe imetangazwa (Promotion)/ imeonyeshwa katika kumbi za Sinema;
  • Filamu iwe na urefu kuanzia dakika 40;
  • Filamu iwe imetumia lugha nyingine mbali na kiingereza kwa Zaidi ya 50%, ikiwa na Subtitles za kiingereza;
  • Filamu iwe katika muundo wa Digital Cinema Package (DCP) kwa ubora wa angalau 2040 kwa 1080 pixels (2K);

Filamu iwe na sauti ya kipimo cha 5.1 au 7.1, au iwe nyenye chaneli 3 za Sauti (left, right & centre).

Angalizo: Filamu ambazo zilisambazwa au kufanyiwa maonyesho nje ya kumbi za Sinema hazikidhi vigezo kwenye Tuzo hizi. Maonesho hayo kwa umma ni:

  • Filamu kuonyeshwa kwenye Cable Telesheni;
  • Filamu isiwe katika PPV (Pay-Per-View) Video in Demand;
  • Filamu isiwe kwenye usambazaji wa DVD; na
  • Filamu isiwe imeonyeshwa/ imesambazwa kwenye ndege.
  • Kusambaza kwenye mtandao wa Internet.

Waandaaji waFilamu nchini wanaalikwa kuwasilisha filamu zinazokidhi vigezo vya ushiriki wa Tuzo hizi za Oscars ili ipatikane filamu moja itakayowasilishwa kwa waendeshaji wa Tuzo hizo nchini Marekani.

Tarehe za kupokea Filamu

Kamati itaanza kupokea filamu kuanzia tarehe 10 Agosti, 2023 hadi Tarehe 15 Septemba, 2023. Link za filamu zitawasilishwa kupitia: tanzaniaoscars@gmail.com. Kwa taarifa Zaidi, tembelea: Tanzania_oscars @instagram, @twitter, @facebook

NB: Kwa Maoni au Maswali Tafadhali tuma Baruapepe kwenda: tanzaniaoscars@gmail.com

 

imetolewa na

Dkt Mona Mwakalinga
Mwenyekit wa Kamati
10/08/2023