Abdallah Nzunda | Mkojani
Baada ya mihangaiko na uchovu wa siku nzima wengi huwa wanapenda kuchukua muda wao wa kupumzika kutizama vichekesho kama vitu vinavyo waburudisha na kuwafanya wapunguze mawazo na kusahau masaibu waliyokumbana nayo kutwa nzima, Hapa kwetu kuna wachekeshaji wengi sana na kila mmoja ana aina yake mfano nikisema “Ngo’ombe weweeee!.
Tayari unajua unajua ni mtu gani nataka kumzungumzia, Sasa leo kwenye kipindi cha sura tofauti tunamuangazia Muigizaji maarufu mchekeshaji na pendwa hapa nchini, Abdallah Nzunda au maaarufu anajulikana kama Mkojani Bin Daruweshi, tutaangalia Filamu na Tamthilia alizoigiza kuanzia wakati anaitwa kipupwe hadi kufika kwenye jina la Mkojani. Ungana nami mwanzo hadi mwisho.
Kunguru Hafugiki 2016
Mwaka 2016 Abdallah Nzunda aliigiza kwenye filamu ya Kunguru Hafugiki, Akitumia jina la Kipupwe ambalo aliigizia husika ya Baba Mwenye nyumba na kuburudisha watu kutokana na maneno yake aliyokuwa akiyatumia, ni ya kuchekesha na kuburudisha mno.
Narudi Jela 2020
Mwaka 2020 Abdallah Nzunda aliigiza Filamu ya Narudi Jela ambayo alitumia husika ya Mkojani, Mkojani ni husika inayoonesha tabia za watu wa Pwani ambao haswa ni watu wenye mambo ya Kiswahili lakini pia wanajihusisha na mambo kama Uchawi, na Husika hii ilmpa umaarufu mkojani katika Filamu hii akiwa kama Mjomba anae amua kuuza mali za Mtoto wa dada yake ambae yupo jela. Kama hujaitizama Filamu hii inapatikana Youtube.
Pusha 2020
Mwaka 2020 aliigiza Filamu ya Pusha ambayo alitumia husika ya mkojani akiwa kama Mjumbe serikali ambae anapinga matumizi ya bangi kwa vijana kwa kuwa yanafanya vijana waharibikiwe kitabia na kimuonekano, kwenye kwenye Filamu hii kuna burudani nyingi sana alizozifanya na kuburudisha.
Binamu 2021
Binamu ni Filamu ambayo Mkojani alicheza husika ya Mjomba ambae anajaribu kumrekebisha Binamu yake lakini ni moja ya Filamu zenye burudani ndani yake na alifanikiwa kuwakilisha vizuri husika yake,
Kubwa Kuliko 2021
Hii ni Filamu nyingine ambayo Abdallah Nzunda alicheza kama Bashilu ni moja kati ya husika nzuri ambayo aliigiza, Bashilu alikuwa ni mtu mwenye asili ya kiarabu na kipemba lakini ni mtu anaeamini kwenye majini na uchawi, husika hii ilifanikiwa kuleta mafanikio mazuri kwani haikuwa na kuchekesha sana bali ni kutisha na kuwa na asili ya mkazo na kupelekea watu kumuona Bwana abdalah Nzunda kucheza husika ya tofauti.
Buti La Jeje 2020
Mwaka 2020 katika husika ya Mkojani aliigiza Filamu ya Buti la Jeje ambayo acheza kama Mwenye nyumba. Filamu hii alicheza vizuri na kuburudisha kutokana na misemo yake aliyokuwa akiongea, kitu kingine ni kwamba husika ya Mkojani ni aina ya husika zenye matambo na kujigamba ilihali haina uweza wa kumudu hata chembe ya ugomvi,
Govinda 2020
Filamu ya Govinda yam waka 2020 ni Filamu ambayo Mkojani aliigiza huku akitumia husika yake ya Mkojani, akiwa kama Mjomba anae wafanyia tohara au jando vijana, na kuwapa somo kuhusu Maisha ya Mwanaume na mwanamke na kuwatengenezea misimamo, kwenye Filamu hii utaburudika kwa ucheshi na manen ya kuburudisha unaweza kuitzama Filamu hii Youtube.
Kujiongeza 2020
Mwaka 2020 Abdallah Nzunda aliigiza kwenye Filamu ya Kujiongeza ambayo alitumia jina la Mkojani na husika hii ikaendelea kupendwa na watu kutokana na burudani za kuchekesha pamoja na visa vilivyokuwa vikitokea ndani yake, akiwa kama Boss anae waajiri vijana na kuwambia wasizubae wajiongeze kwenye kazi wanayofanya na kwenye kila kitu, Ukitizama Filamu hii utaburudika sana.
Mkufu 2023
Ndani yam waka 2023 Abdallah Nzunda ameigiza kwenye Filamu ya Mkufu hii ni Filamu ambayo utaona jinsi ambavyo husika ya Mkojani ambayo aliitumia ilifanya vizuri na bad ikiendelea kuburudisha na kusisimua mno, akiwa kama mwenyekiti anaingiwa na tamaa nakuungana mmiliki wa chombo cha moto kumdhurumu dereva wa chombo hicho. Ni moja ya Filamu ya kusisimua na kuburudisha na kuelimisha pia si ya kukoa kuitizama.
Filamu ipi kati ya hizi umeitizama na kupenda jinsi Mkojani alivyocheza husika yake, Tuandikie kwenye Comment, pia usisahau ku subscribe na kugusa alama ya kengele ili uwe wa kwanza kupata taarifa zetu zote.