Karibu CineBox, Hizi ni Tamthilia zilizofanya vizuri katika vipindi vya televisheni mwaka 2022, Tamthilia hizi zenye Maudhui yaliyo na mafunzo ndani yake ya kuelimisha jamii,  pamoja na visa mbalimbali kutoka kwa wahusika tofauti tofauti, walicheza kwa viwango vikubwa.

10.       Fundi

Hii ni moja kati ya tamthilia mpya na zilizo pekelewa vizuri na watu kwa sababu ya kufuatiliwa baada ya kutoka, Tamthilia ya Fundi ni tamthilia inayohusu Mafundi wawili ambao wanakutana na visanga kutoka kwa wateja wao katika maisha yao ya Ufundi mmoja akiwa ni Fundi nguo na mwengine ni fundi seremala,

Lakini pia ni Tamthilia yenye maudhui yenye kuonyesha baadhi ya tabia zinazofanywa na Mafundi wengi katika jamii zetu, Na kupelekea Ugomvi na kutokuelewana na watu vizuri kutokana na kutotimiza kazi kwa wakati za wateja wao, Tamthilia hii inapatikana ndani ya chaneli ya Sinema Zetu kupitia king’amuzi cha Azam Tv.

9.       Mwali

Hii ni Tamthilia mpya iliyoanza hivi karibuni ndani ya Maisha Magic Bongo na ambayo imepokelewa na watu na kuanza kufuatiliwa, Tamthilia ya Mwali ni tamthilia iliyobeba Mudhui ya kuitamaduni wa kiafrika kuanzia kwenye mambo ya Utawala wa ki chifu, Mila na Desturi za zamani, pia kuonyesha upande wa ndoa za zamani zilivyokuwa zikifanywa katika utaratibu wake,

Tamthilia ya mwali imeonyesha upande wa familia za kuitawala jinsi zinavyoingia katika misukosuko na baadhi ya watu wanaotaka kudondosha himaya ya kiongozi husika kama mtoto wa nje wa Chifu (Semindu) kugombana na Baba yake Chifu KandaMsile akitaka yeye awe ndie mtawala wa Boma, Unaweza kutizama Tamthilia hii ndani ya Maisha Magic Bongo kupitia Dstv.

 

8.       Pazia

Ni tamthilia yenye mtiririko mzuri wa visa kwa wahusika wake katika tamthilia hiyo kuna matukio mbalimbali ambayo huwa yanatokea katoka Familia na jamii zetu kwa ujumla ndani ya tamthilia ya Pazia kuna Maisha ya wivu, chuki, na visa mbalimbali vya uswahilini kama Bidu pamoja na Mke wake kuzozana kila siku kwenye ndoa yao.

Lakini pia tamthilia hii imeteuliwa kuwania Tuzo kwenye kwenye kipengele cha Muigizaji bora chaguo la mashabiki pamoja ni muigizaji bora wa kike kupitia Tuzo za Tanzania Film Festival Awards, Tamthilia hii pia imeonyesha Usaliti baina ya wana ndoa ambao mwisho wake unaweza kupelekea hata umauti kama Mama Groria na mwanae walivyokuwa wakimgombania mwanaume mmoja kuwa nae kimapenzi. Tamthilia hii pendwa inapatikana ndani ya Maisha Magic Bongo kupitia Dstv.

7.       Maji Ya Shingo

Katika orodha ya tamthilia zinazo fatiliwa na watu basi siwezi kukosa kuitaja Maji ya Shingo kwani ndani ya mwaka 2022, Maji ya shingo imezidi kufatiliwa na kupendwa haswa katika mpangilio wa kimatukio kwenye tamthilia hii kuna husika za watu mbalimbali na kila mmoja anapitia maisha ya aina yake ,

Lakini pia ni tamthilia yenye burudani sana Filamu hii imebeba matukio ambayo tunakutana nayo kila siku kwenye jamii zetu kama Wizi, Chuki, na kadha wa kadha, Usikose kufatilia Tamthilia hii ndani ya Sinema Zetu kupitia king’amuzi cha Azam Tv.

6.        Chini Ya Kapeti

Hii ni Tamthilia pendwa ndani ya Chaneli ya Sinema Zetu ndani ya Azam Tv, Tamthilia hii ilifanya vizuri mwaka 2022, kutokana na watu kuifatilia pia ilifanikiwa kuchaguliwa kuwania Tuzo za Tanzania Film Festival Awards mwaka 2022, kwenye kipengele cha Muigizaji bora chaguo la Mashabiki,

Ni Tamthilia iliyobeba Matukio au stori zinazo wahusu wahusika katika maisha yao ya kila siku, pia ni tamthilia ambayo ndani yake imeonyesha maisha ya uswahilini na harakati za mtaani, kwa upande wa vijana jinsi wanavyotafuta mkate wao wa siku kwa kuiba na kupora, ni tamthilia ilikuwa na matukio yanayotokea nyuma ya pazia katika upande wa mahusiano pamoja na maisha kwa ujumla endelea kuifatilia ndani ya Sinema Zetu.

5.         Huba

Tamthilia ya Huba ni moja kati ya tamthilia kongwe ambayo imeanza kuruka tangu mwaka 2017 ndani ya Miasha Magic Bongo na imezidi kuwa nzuri siku hadi siku ni tamthilia iliyobeba wahusika walio onyesha uwezo wao wa kuigiza na kufanya iwe tamthilia inayofatilia na watu hadi sasa mwaka 2023, Tamthilia hii imebeba stori nzuri inayohusu mambo mbalimbali ambayo tunakutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku kama vile Mapenzi , Chuki pia ugumu wa maisha kupelekea watu kufanya biashara ya kujiuza ili kupata pesa ya kujikimu, kama ilivyotokea kwa Happy baada ya kuingia kwenye mahusiano na JB mtu mwenye pesa zake na kujikuta ana msahau na kumkata mume wake, Usikose kufuatilia tamthilia hii nzuri ambayo unaipata ndani Maisha Magic Bongo kupitia Dstv.

4.         Yalaiti

Ni tamthilia yenye stori nzuri ambayo imebeba wahusika tofauti wanaokutana na matukio mbalimbali katika maisha yao ya kila siku matukio yaliyojawa  Wivu, Chuki, Mapenzi, Tamthilia hii iliteuliwa kuwania Tuzo za Tanzania Film Festival, Kwenye kipengele cha Best Actress mwaka 2022,

Pia hii ni moja kati ya filamu ambayo inafatiliwa na watu kwa sababu ya mtiririko visa mfano fumanizi la Remmy kukutwa na Stella msibani pamoja na momo kulazimisha kutoka mume wa mtu, haya ni baadhi ya kati ya mengi ambayo tumeyaona katika tamthilia hii ya Yalaiti, Hivyo usikose kuifatilia tamthilia hiyo inayoruka kupitia Maisha Magic Bongo ndani ya Dstv.

 

3.        Kitimtim

Hii ni Tamthilia ya Uchekeshaji au Comedy Series ambayo imefanya vizuri ndani ya mwaka 2022, Tamthilia hii imezidi kupendwa kutokana na wahusika kucheza vizuri na kutoa burudani ya kufurahisha watu, Tamthilia hii imeteuliwa kuwania Tuzo ya Best Comedy mwaka 2022 kwenye Tuzo za Tanzania Film Festival, Pia baadhi ya matukio ya kwenye Tamthilia hii yamezidi kuifanya izidi kupendwa na kufuatiliwa na watu zaidi,

Mfano tukio la Tin White au Zunde alipokuwa amerudi nyumbani alishangazwa baada ya kukutana na wanawake kama sita wanaofanana sura na kila mmoja akiendelea na shughuli  zake, hivi ni baadhi ya visa na vimbwanga vilivyotokea usikose kuendelea kuifatilia ndani ya Maisha Magic Bongo kupitia Dstv.

 

2.         Kombolela

Hii ni Tamthilia pendwa ambayo ilikuwa inafatiliwa na watu, pia ni Tamthilia ambayo imejizolea Tuzo pamoja na kushinda Tuzo mwaka 2022, kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume, ambae ni Mzee N’Kwabi Ng’wanamala Tamthilia ya kombolela imebeba maudhui mazuri na kuonyesha maisha halisi ya Uswailini ambayo tunayaona kwenye jamii zetu,

Kombolela ni Tamthilia ambayo husika zake zimechezwa katika ubora wa aina yake na kupelekea kushinda Tuzo mbalimbali.

 

1.         Juakali

Ni tamthilia ambayo imefanya vizuri ndani ya mwaka 2022, kutokana na kubeba stori ambayo imemuhusisha kila mshiriki katika tamthilia hiyo kulingana na husika zao, Juakali ni tamthilia iliyopata mafanikio makubwa na kupelekea mwaka jana muongozaji waTamthilia hiyo Lamata kuibuka mshindi kwenye Tuzo za Tanzania Film Festival Awards kipengele cha Muogozji bora wa kike mwaka 2022, pamoja na Tuzo ya Muigizaji bora kike chaguo la watazamaji,

Pia ndio tamthilia ambayo imeshirikisha waigizaji wakubwa maarufu kutoka mataifa mbalimbali, kama vile Van Vicker, Show Madjozi, Richard Mofeda pia tamthilia imezidi kupendwa zaidi kutokana mtiririko mzuri wa matukio kwa wahusika mfano Luka church boy kupata faraja kwa Femi baada ya kuteseka kwa Maria kwa muda mrefu. Usikose kuifatilia inapatikana Dstv ndani ya Miasha Magic Bongo.

Na hizo ndizo Tamthilia ambazo zilifanya vizuri ndani ya mwaka 2022 na zingine zinaendelea kufanya vizuri mwaka 2023, Tamthilia hizi pia zimepata mafanikio ikiwemo kushinda baadhi ya Tuzo ndani na nje ya nchi, Kama kuna tamthilia nzuri unayoifahamu iliyofanya vizuri mwaka 2022, tuandikie kwenye sehemu ya comment, Asanteni.