Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hyat Regence Jijini Dar es Salaam, ukihusisha waandishi wa habari na wadau wa filamu Tanzania katika uzinduzi wa tamthilia mbili mpya, ”Mtaa wa Kazamoyo” yakwake Dr Cheni na ”Lolita” ya william Mtitu,  zitakazoanza kuonekana Agosti 04 na Agosti 14 mwaka huu zikichukua nafasi za tamthilia, “ Fungu langu” na ”Jeraha” zinazorushwa kupitia kisimbuzi cha Azam ndani ya chaneli pendwa ya Sinema zetu.

Huku tamthilia hizo mpya zikisheheni watu wengi maarufu wa tasnia hiyo ya uigizaji wakiwemo Denis Komba ,Chris Mziwanda, Genevieve Nnaji, Careen Simba na Angle Dickson kwenye  “Lolita”, na vile vile kwa upande wa “Mtaa wa Kazamoyo” imehusisha watu kama Dr Cheni, Nyama Yao na Amina Ahmed.

Moja ya mtayarishaji wa kazi hizo, Dr cheni, alisema kwamba haikuwa rahisi kupeleka kazi Azam Tv kwa kuwa iliwabidi wafanyie marekebisho kidogo ya kazi yao, ili kukidhi maadili na utamaduni wa kitanzania. Pia aliwahasa wakongwe katika filamu kuwapa nafasi vijana ili waweze kuonesha vipaji vyao.

Kwa upande wa Azam Tv, mkuu wa chaneli ya simema zetu Sophia Mgaza  aliendelea kutoa rai kwa waandaaji waweze kuhakikisha wanasimamia ubora wakazi zao, huku Azam Tv ikijipanga kuanza kupokea filamu kutoka kwa watayarishaji na waandaaji wa kazi hizo kupitia mfumo rafiki utakao tangazwa hivi karibuni.