Washindi Tamasha la Swahili International film festival mwaka 2023, Swahili International film festival awards ni Tamasha linalofanyika Kwa mwaka mara Moja huko Mombasa Kenya, wafuatao ni washindi wa Tuzo za Siff mwaka 2023

Tuzo ya Filamu bora ya lugha ya Kiswahili ilichukuliwa na Filamu ya Joyce’s Dream kutoka Tanzania.

Tuzo ya Filamu Fupi bora ya mwaka ikachukuliwa na Filamu kutoka Tanzania inayoitwa Kitendawili

Tuzo ya Muongozaji bora wa mwaka ikaenda kwa Mohammed Suleiman Hamadi au Mudi Sule kutoka kwenye Filamu ya Kitendawili.

Tuzo ya Muigizaji Bora wa mwaka ikaenda kwa Alan Ramadhan kutoka kwenye Filamu ya EOINII kutolea Tanzania.

Tuzo ya Best Actress ilikwenda Kwa Sabrina Khamis kupitia Filamu fupi ya Kitendawili.

Tuzo ya Best Supporting Actor ikaenda kwa Habibu Mambo kutoka kwenye Filamu ya EOINII.

Tuzo ya Best Supporting Actress ikaenda kwa Paschalina Silanda kutoka kwenye Filamu ya Fumbuo kutoka Tanzania.

Tuzo ya Best Screenplay ilienda Kwa Sara Kimario kutolea kwenye Filamu ya Fumbuo.

Tuzo ya Ubunifu Bora na uzalishaji ilienda Kwa Ochu Kiota kutoka Tanzania kupitia Filamu ya Fumbuo.

Tuzo ya muundo bora wa mavazi ikaenda kwa King Hasira

Tuzo ya Best Visual Effects ikaenda kwa Eddie Mzale muongozaji wa Filamu ya EOINII.

Na hao ndio washindi walio peperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwenye Tuzo za Siff 2023.

Neno la shukurani kutoka kwa mkurugenzi wa Swahili film festivals

Ninapenda kuchukua fursa hii Kuwapa pongezi nyingi washindi wetu wa mwaka huu, pia napenda kuwapa Moyo wote walio shiriki Mashindano haya, kwakweli tunashukuru sana. Asanteni kwa kutuma kazi zenu Mungu awabariki sana.

Kwa wale ambao hawaja fanikiwa na ushindi ningependa kukuambia amini kwamba wewe ni mshindi tu mana upo katika washindani, endelea kukaza hakika wakati ukifika wa wewe kutuzwa hakuna atakae pinga.

Tanzania Twawashukuru
⁨Muddy Zanzbar⁩-Kitendawili
Sayus Studios Tz⁩
Habib Mambo-Eonii
Kuza Cave
Rinatha Cyriakus-Saviora
Paschalina Silanda-Fumbuo
Sara Kimario- Fumbuo
Eddie Mzale-Eonii
Allan Ramadhan-Eonii
Sabrina Khamisi-Kitendawili

Kenya Twawashukuru

Steve Kipande-Gundu
Stanley Njogu-Rishai
Omar Hamza-Mzigo
Recho Shakes-Nenda
Geoffrey Changa-Corona Chronicle
Amazon Kings

Na wengine wengi tu kwakweli pokeeni hongera nyingi tu kwa ushindi

Na tuzidi kusonga mbele Tunawatarijia mwaka ujao kwa nguvu nyingi na kasi mpya
Asanteni sana na Mungu awabariki.