Ikiwa ni msimu wa 26, wa Zanzibar international film festival awards (ZIFF) 2023, Ziff ni Tamasha kubwa la Tuzo za Filamu, Tamthilia, na mambo kadha wa kadha yanayohusi Sanaa, likiwa linafanyika mara moja tu Kwa mwaka na kukutanisha watu kutoka pande zote za Dunia.

Lengo la Tamasha hili ni kuendeleza na kukuza tasnia ya Filamu barani Africa, na kutoa jukwaa la kubadilishana uzoefu na mawazo katika nyanja ya Filamu, pia Ziff hutoa Fursa ya mafunzo, warsha na midahalo juu ya masala ya Filamu na Sanaa Kwa ujumla.

Wafuatao ni washindi wa Tuzo za ZIFF mwaka 2023 ukanda wa East Africa na Tanzania,

Tuzo ya Filamu bora ya mwaka Tanzania ilichukuliwa na filamu ya  EOINII. Kutoka kwa muandaaji wa filamu Edwin Mzale,

Tuzo ya Muigizaji Bora wa kike ikaenda kwa mwanadada Tunu Mbegu, hii ikiwa ni Kwa mara yake ya pili mfululizo kushinda Tuzo hizi kwenye Tamasha la Ziff, mara ya kwanza alishinda Tuzo ya Best actress katika Filamu ya uncle iliyo ongozwa na Hatibu Madudu na mwaka huu ameshinda Tuzo ya hio kupitia Filamu ya still ok to date iliyo ongozwa na Kefa Hussein.

Tuzo ya Muigizaji bora wa Kiume imekwenda Kwa Isaya Lyoba kutoka kwenye Filamu ya Nakupenda iliyo ongozwa na Juma Sada,

Upande Filamu bora ya Afrika Mashariki ilichukuliwa na Filamu ya Half Open Window kutoka Kenya iliyo ongozwa na Omar Hamza na kuandaliwa na Wacera Margaret,

Tuzo ya Muigizaji Bora wa kiume wa mwaka 2023 Africa Mashariki ilienda kwa Dr. Edwin Nyutho.  Pamoja na Tuzo ya Muigizaji Bora wa kike ilikwenda Kwa Grace Wacuka kutoka Kenya kwenye Filamu ya Married to Work.

Filamu tatu zilifanikiwa kushinda Tuzo za Sembene Ousumane.

Ikiwemo Filamu Fupi ya Katope kutoka Tanzania iliongozwa na Walt Mzengi pamoja na Filamu ya Mawimbi kutoka Kenya na Neb Tawy kutoka Egypt.

Filamu zilizopewa heshima au special mention ni Filamu kama Act of Love ya Kenya iliyoandaliwa na Erick mwangi, Filamu ya 9Memeza ya South Africa iliyoandaliwa na Sithembiso Mathenjwa, Filamu ya Citizen Kwame ya nchini Rwanda iliyo ongozwa na Yuhi Amuli, pamoja na Filamu ya Ziwa Uganda ya Samuel Tibandeke.

Kubwa kati ya yote ni kuwa ZIFF Ilikuwa na  mabalozi wanne tu, Duniani Kwa miaka yote 26 na Jana wameongeza balozi wao mwingine aneitwa Manfredo fanti ambae alipokea zawadi yake ya utambulisho wa kibalozi huko ngome kongwe kwenye nchi ya majahazi.